PRESHA YA MACHO INAVYOWEZA KUSABABISHA UPOFU.

Na Jacqueline Benson. PRESHA ya macho ni mingoni mwa maradhi ambayo yanaweza kumsababishia mtu kupata upofu wa kudumu endapo hatapatiwa tiba mapema. Magonjwa hasa yanayoshambulia mtoto wa jicho na uoni hafifu yanaweza kumuathiri mtu kulingana na mfumo wake wa maisha na umri huku baadhi ya magonjwa kama kisukari na kisonono yanachangia maradhi haya kwa kiasi kikubwa na kusababisha ulemavu wa macho . Ugonjwa wa kisukari pamoja na kisonono huweza kusababisha ugonjwa wa macho na matatizo mengine kutokana na kushusha kinga ya mwili(chembe hai nyeupe) na kutengeneza mazingira rahisi ya mwili kushambuliwa. Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho na Upasuaji wa retina kutoka Hospitali ya Agarwal’s Dar es Salaam, Dk.Emeritus Chibuga alisema kuwa presha ya macho ni ugonjwa unaotokana na kutokuwa na uwiano kwenye mfumo unaotengeneza na kutoa maji kwenye jicho . Dkt Emeritus aliongeza kuwa kiasi cha utengenezaji wa maji katika...