POLISI ZANZIBAR WAMSHIKILIA MTUHUMIWA WA ULAWITI

Na Abdulrahim Shekhe.

Jeshi   la   Polisi   visiwani   Zanzibar  linamshikilia  mtuhumiwa  wa  kesi  ya  ulawiti  Hassan  Aboud  Talib   maarufu  kwa  jina  la  ‘Kiringo’  kwa  kosa  la  kumlawiti mtoto  mwenye   umri   wa   miaka   13   jina   limehifadhiwa.


Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa  mjini  magharibi  Hassan  Nasri  alidhibitisha kukamatwa  kwa  mtuhumiwa  huyo mwenye  umri  wa  miaka  45  na amepelekwa  kwenye  kituo  cha  polisi  Fuoni  mjini  Unguja .
“Ni  kweli   Kiringo   tumemkamata  na  yupo  kwenye  mikono  ya   jeshi  la  polisi  kwasasa   yupo   kwenye  kituo  cha Fuoni  ,tunaendelea  na uchunguzi  tayari  nishaunda  timu  ya  upelelezi  itakayolifanyia  uchunguzi  suala  hili  .Nimewachagua  wakuu  wa  upelelezi  kutoka  wilaya  zote  tatu  za  mkoa  wa  Mjini  Magharibi , na  nawaomba   wananchi  wawe  na  subra  na  niwahakikishie  tu  kesi  itakwenda  mahakamani  pindi  tu  taratibu  zitakapo  kamilika ” alisema  kamanda  Nasri.


Kiringo  ambaye  pia  ni  mfanyakazi  kigogo  wa  mamlaka  ya  mapato  Tanzania TRA  kanda  ya  Zanzibar  amekuwa  akishtumiwa  na kuhusishwa  mara   kadhaa  na  wananchi  wa  Zanzibar  kuhusika  na  vitendo   hivyo  vya  kinyama  visiwani  humu.

Kwa  upande  wake  makamo  mwenyekiti  wa  Baraza  la vijana  wilaya ya  mjini   Francisca  Clement  alieleza kusikitishwa  na  tukio hilo  “nilipata taarifa majira ya saa nne  asubuhi nilipouliza nani muhusika niliambiwa Kiringo  ,nilisikitika sana maana hii si mara ya kwanza kufanya haya mambo naliomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa huru ili ikibainika afikishwe kwenye vyombo  vya  sheria” alisema  Francisca

Comments

Popular posts from this blog

PRESHA YA MACHO INAVYOWEZA KUSABABISHA UPOFU.