PRESHA YA MACHO INAVYOWEZA KUSABABISHA UPOFU.
Na Jacqueline Benson.
PRESHA ya macho ni mingoni mwa maradhi ambayo yanaweza
kumsababishia mtu kupata upofu wa kudumu endapo hatapatiwa tiba mapema.
Magonjwa hasa yanayoshambulia mtoto wa jicho na uoni
hafifu yanaweza kumuathiri mtu kulingana na mfumo wake wa maisha na umri huku
baadhi ya magonjwa kama kisukari na kisonono yanachangia maradhi haya kwa kiasi kikubwa na
kusababisha ulemavu wa macho.
Ugonjwa wa kisukari pamoja na kisonono huweza
kusababisha ugonjwa wa macho na matatizo mengine kutokana na kushusha kinga ya
mwili(chembe hai nyeupe) na kutengeneza mazingira rahisi ya mwili kushambuliwa.
Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa magonjwa
ya macho na Upasuaji wa retina kutoka Hospitali ya Agarwal’s Dar es Salaam, Dk.Emeritus Chibuga alisema
kuwa presha ya macho ni ugonjwa unaotokana na kutokuwa na uwiano kwenye mfumo
unaotengeneza na kutoa maji kwenye jicho
.
Dkt Emeritus aliongeza kuwa kiasi cha utengenezaji
wa maji katika jicho ni wa kawaida ila yanayotoka huwa ni kidogo jambo ambalo
husababisha mkandamizo wa retina kutokana na wingi wa maji.Mpaka kufikia hatua
ya kuitwa presha ya jicho Dk.Emeritus alieleza kuwa tayari mishipa ya fahamu unaomwezesha mtu kuona imekwisha
kuharibika kutokana na maji maji hayo.
Utengenezaji
wa maji haya ni muhimu kutokana na kusafirisha virutubisho katika seli
zilizo ndani ya jicho na kuwezesha upatikanaji wa hewa safi ndani ya macho.
Kutokuwepo kwa uwiano wa utengenezaji na utoaji wa maji kunasababishwa na
kuziba kwa mirija inayohusika na utoaji wa maji hayo na kupelekea jicho
kupoteza uwezo wake wa kuona.
Comments
Post a Comment